User talk:Collinsalex2

From Wikimedia Commons, the free media repository
Jump to navigation Jump to search
Welcome to Wikimedia Commons, Collinsalex2!

-- Wikimedia Commons Welcome (talk) 13:23, 1 March 2020 (UTC)[reply]

Mwaliko wa kutoa maoni yako kuhusu Mwongozo wa Kimataifa wa Mwenendo na Nidhamu

[edit]

Habari ndugu Mwanawikipedia!

Mimi ni mwezeshaji wa mradi uitwao Mwongozo wa Kimataifa wa Mwenendo na Maadili. Ni mradi mchanga/mpya ambao Shirika la Wikimedia Foundation linanuia kuuanzisha endapo wadau wataona ni mradi unaofaa na kuunga mkono wazo hilo. Nakukaribisha usome mwongozo huo na kisha utoe maoni yako kwa kujibu maswali yote au baadhi yake kwa yale utakayopenda kuyatolea maoni HAPA

Taarifa zaidi kuhusu Mwongozo wa Kimataifa wa Nidhamu na Mwenendo

Shirika la Wikimedia Foundation lina mpango wa kuanzisha Mwongozo wa Kimataifa wa Mwenendo na Maadili. Lengo la mwongozo huo ni kujaribu kuoanisha vitu vya msingi vya kimwongozo vinavyopatikana katika miongozo midogo midogo iliyopo tayari katika kila jamii husika (mfano katika Jumuiya yetu hii ya wahariri wa Wikipedia ya Kiswahili). Lengo hasa la mwongozo huu ni kujaribu kutengeneza mazingira ambayo wanawikipedia wote duniani watakuwa na uelewa wa pamoja juu ya vitu vya msingi kuhusu nini kinakubalika na kipi hakikubaliki wakati wa uchangiaji (uhariri) au utumiaji wa Wikipedia, na pia pale wanawikipedia wanapowasiliana ndani ya tovuti ya Wikipedia yenyewe au wanapokutana ana kwa ana katika warsha na mikutano mbalimbali ya Wanawikipedia. Wazo hilo limekuja baada kutokea kwa baadhi ya matukio kwa baadhi ya Wanawikimedia anbapo katika tafiti iliyofanywa mwaka 2015 , ilionekana baadhi ya Wanawikimedia walikuwa wakikumbana na unyanyasaji wa kitabia (mfano matusi, kuitana majina yasiyofaa, kutishiana n.k) na Wanawikimedia wenzao, hivyo kuwakatisha tamaa ya kuendelea kuchangia katika miradi ya Wikimedia.Wewe kama mdau muhimu katika miradi ya Wikimedia Foundation, unakaribishwa ku soma zaidi kuhusu mwongozo huona unaweza ku toa maoni yako Hapa kabla ya tar 29th April 2020.

Mwaliko wa kujiunga na kundi la Wahariri wa Wikipedia

Nakukaribisha ujiunge na kundi la Wahariri wa Wikipedia kutoka Tanzania (Dar es Salaam) ili tuweze kujadiliana na kubadilishana mawazo, uzoefu na mambo kadha wa kadha kuhusu Uhariri wa Wikipedia na miradi mingine yake ya Wikimedia Foundation. Iwapo utapenda kujiunga, usisite kuwasiliana nasi kupitia wikitzagroup@gmail.com, na kwa taarifa zaidi kuhusu kundi la Wahariri wa Wikipedia wa hapa Dar es Salaam na Tanzania kwa ujumla kuhusu miradi waliyoifanya tayari, unaweza tembelea hapa ukurasa wao wa meta uitwao Wikimedia Community User Group Tanzania au pia katika Facebook kwa jila la Wikimedia Tanzania.

Ndimi Mtavangu19:09, 18 April 2020 (UTC)[reply]